Na magdalena Kashindye -KAHAMA
Chama cha mapinduzi (CCM) wilayani Kahama mkoani Shinyanga kimesema hakina taarifa ya urejeo wa James Daud Lembeli katika chama hicho kutokana na kushindwa kufuata taratibu na katiba ya chama.
Akizungumza na Mpekuziblog ofisini kwake katibu mwenezi wa CCM wilayani ya Kahama Joachim Simbila amesema chama kimesikia urejeo wa Lembeli lakini hakuna taarifa rasmi iliyothibitishwa, hivyo alichokifanya ni kuutangazia umma kuwa amehama kutoka Chadema kujiunga na CCM.
Simbila amesema katiba ya chama inasema mwanachama aliyehama chama na kurudi kwa mara ya pili anatakiwa kujaza fomu ambayo itaidhinishwa na tawi la eneo analoishi ambapo wao kama viongozi baada ya kusikia taarifa hizo waliwasiliana na uongozi wa eneo husika lakini hakuna taarifa za James Daud Lembeli kujaza fomu
Pia Simbila amesema mkutano aliouandaa James Lembeli haukuwa na viongozi wa chama wilaya sambamba na viongozi wa tawi ambapo katika mkutano huo alikuwepo kiongozi wa serikali ya kijiji kitu ambacho kiongozi huyo hana mamlaka ya kumpokea mwanachama mpya kuingia ndani ya chama.
Daud James Lembeli (mwanamaria) June 13, 2018 alitangaza kuachana na Chadema na kurejea chama cha mapinduzi CCM ambapo alisema ameachana na siasa za majukwaani kwani wazazi wake wote ni waasisi wa TANU ambacho kiliunda CCM hivyo yeye kuwa chama cha upinzani ni kuwakataa wazazi wake