Daimond Awatolea Uvivu Timu Zari na Mobetto "Msiniletee U-team kwa Watoto Wangu"

Daimond Awatolea Uvivu Timu Zari na Mobetto "Msiniletee U-team kwa Watoto Wangu"
Msanii wa Bongo Fleva Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz kupitia akaunti yake ya Instagram amesema habagui watoto wake na wala hapendi mambo ya utimu. Kupitia akauntihiyo ameweka picha akiwa na mwanaye Daylan na kuandika:

“His is my Kid and he will forever be my Kid, tena My Beloved Kid, na si vinginevyo. Halafu cha kuongeza, msiniletee U-team wenu kwa watoto wangu! they are all my Kids, Nawapenda na siwezi mtenga wala kumbagua yeyote,”

Diamond Platnumz ni baba wa watoto watatu, watoto wawili ‘Tiffah na Nillan’ akiwa amezaa na Zari The Boss Lady na mtoto wa mwisho, Daylan akiwa amezaa na Hamisa Mobeto.

Kitendo cha Mobeto kuzaa na Diamond wakati mwimbaji huyo bado alikuwa na mahusiano na Zari,  kilipelekea warembo hao kuanza kurushiana maneno mitandaoni,  kitu kilichozaa kile kinachoitwa Team Hamisa na Team Zari.

Top Post Ad

Below Post Ad