Davido Kupanda Juu y a Stage Moja na Jay Z

Davido Kupanda  Juu y a Stage Moja na Jay Z
Time hii ni ya msanii Davido kutokea Nigeria kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha la Made in America akiwa sambasamba na Jay Z katika stage moja ikiwa mwaka jana 2017 Wizkid, Tiwa Savage, Maleek Berry pamoja na Mr Eazi walipata nafasi hiyo.

Tamasha hilo litafanyika September 1 -2,2018 Philadelphia, Marekani katika ukumbi wa Benjamin Franklin Parkway ambapo staa huyo ametajwa kwenye list ya wasanii watakao’perform katika tamasha hilo akiambatana na wasanii maarufu kama Meek Mill, Nicki Minaj, Miguel, Janele Monae,Ty Dolla $ign na wengine wengi.



Tamasha hilo la Made in America ni tamasha kubwa ambalo hufanyika kila mwaka nchini Marekani na lilianzishwa mwaka 2012 na Rappaer mkongwe wa Hip Hop Jay Z.

Staa Davido atakua msanii pekee kutokea Nigeria atakayeliwakilisha Bara la Afrika katika tamasha hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad