Dully ni 'Mshenzi' - Master J


NA FATUMA MUNA
Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa Bongo fleva, Joachim Kimario ‘Master J’ amefunguka na kumshukuru Msanii Dully Sykes kwa kuufanya wimbo wa Dhahabu kuwa mkubwa ingawa ni 'mshenzi'.


Master Jay ameyasema hayo akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa, wakati akisimulia namna ambavyo wimbo wa 'dhahabu' uliofanywa na Dully akiwa amemshirikisha Joseline na Mr. Blue ulivyorekodiwa.

"Wakati wa natengeneza wimbo wa 'Dhahabu' Dully  alinitesa sana siku hiyo. Kwanza alikuja studio na totoz mbili alafu ananukia mno nikampa beat aifanyie kazi,  Duly wewe ni mshenzi sana. Alirekodi wimbo mzima mic ikiwa imegeuka nyuma, alipomaliza akanambia Master hiyo itakutosha halafu akaondoka zake na totoz zake," Master J

Ameongeza kwamba "Nilihangaika sana mpaka hizo sauti mnazisikia hivo. Namshukuru Mungu, Mungu mkubwa wimbo ulikuja kuwa mkubwa. Huyo ndiyo misifa, Namshukuru alinipatia 'hit song"

Mbali na hayo Master Jay amesema kwa sasahivi wasanii wanashindwa kutengeneza nyimbo kali kutokana na watu wengi hawaangalii vipaji.

Top Post Ad

Below Post Ad