Ghasia ageuka 'Mbogo' bungeni, asema 'hatukubali'


NA FATUMA MUNA
Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia amedai kuwa kuna wabunge wamekaa vikao na kuandaliwa kwenda kuwadhalilisha  wabunge wanaowatetea wakulima katika mabadiliko ya sheria ya zao la korosho.


Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia.

Ghasia ameyasema hayo, katika mjadala wa bajeti ya Serikali mapema leo ambapo ameweka wazi yeye pamoja na na wabunge wengine wa kusini watahakikisha wanapambana kuwapigania wakulima wa zao hilo.

Ghasia amesema kwamba anafahamu vipo vikao vilivyokaliwa kwa ajili ya kuja kuwadhalilisha wabunge watakao watetea wakulima kuhusu suala la kilimo cha korosho kwa ujumla na kuwataka wakulima kufahamu wabunge wao wapo imara na watawatetea kwa kadri itakavyowezekana.

“Wabunge wote tuna haki sawa za kutetea wananchi wetu, anayetoka katika pamba atetee pamba, anayetoka katika madini atatetea madini yake na anayetoka katika korosho atatetea wa korosho. Niwahakikishie wakulima wanaolima korosho wabunge wao tutapambamba na hata haki isipopatikana ila tutawatetea,"Ghasia.

"Tunaambiwa sisi wabinafsi, korosho inalimwa kwa kiwango kikubwa na mikoa miwili au mitatu lakini tulipokaa katika kamati tukakubaliana na kwenda mikoa 17. Leo tunaambiwa sisi wabinafsi, kuna watu wanakuja kusimama wanasema wanaijua korosho kuliko sisi. Mimi utafiti wangu wa shahada ya kwanza na ya pili inahusu korosho. Leo mtu anakuja humu anaijua korosho na ninasema kila mtu atetee lake na wananchi mjiandae kuwasikia.”

Mbali na hayo Mh. Ghasia amesema kwamba kazi ya serikali ni kuwashughulikia waliofanya ubadhirifu, na kwamba hata kama ni "Hawa Ghasia nipelekeni mahakani lakini siyo kusema wabunge wa kusini wabinafsi".

Mbali na hayo, Mbunge amesema kipindi cha gesi aliijua nia ya serikali na ndiyo maana alikuwa mstari wa mbele hali ilimfanya mpaka kumpoteza baba yake mzazi, kuchomewa nyumba na kuharibiwa mali lakini katika suala la korosho  hayupo tayari.

EATV
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad