Gigy Money Afunguka Mazito Kuhusu Mwanaye "Daimond ndo Baba wa Mtoto"

Gigy Money Afunguka Mazito Kuhusu Mwanaye "Daimond ndo Baba wa Mtoto"
Bado ni drama tele kwa upande wa msanii wa muziki Bongo na video vixen, Gigy Money kuhusu baba mzazi wa mwanae.

Hii ni baada ya kueleza mtoto si wa aliyekuwa mpenzi wake wa siku zote, Mo J. Kila mara anapoulizwa hujibu kuwa baba wa mwanae ni msanii Diamond Platnumz.

Time hii Gigy Money ameendeleza kile alichokianza toka mwanzo kuwa Diamond ndiye baba wa mwanae.

“Sasa Diamond ndio baba mlezi, yaani kama kuna baba ubatizo, Diamond ni baba yake, lazima awe baba yake. Sasa Bongo hii baba mwingine atakuwa nani jamani, Chibu ila baba yake phisically, biologically ni huyo,” Gigy ameiambia Wasafi TV.

Gigy Money ameongeza kuwa tangu alipomueleza Mo J kuwa mtoto si wake hamuhudumii tena na hata mawasiliano hawana kwa sasa. Gigy alijifungua usiku wa kuamkia April 27, 2018 mtoto wa kike.

Top Post Ad

Below Post Ad