Gigy Money Akiri Kutomjua Baba wa Mtoto Wake, Amwangushia Zigo la Kulea Diamond


Gigy alikiri kuwa hamjui baba wa mtoto wake

-Mama huyo wa mtoto mmoja alisema alimchagua Diamond kuwa mlezi wa mwanawe kwa kuwa nyota huyo wa Bongo anajua kuwalea watoto

-Matamshi ya Gigy yalijiri siku chache baada ya kumteama mpenziwe na kumkashifu kwa kuwa na wapenzi wengine

Mcheza densi wa Tanzania Gigy Money alifichua kuwa mwanawe wa kike ni wa msanii maarufu wa Bongo Diamond Platinumz.

Akizungumza na jarida la Dizzim Online, Gigy alifichua kuwa hamjui baba wa mwanawe lakini aliamua kumjata Diamond kama mlezi wa mwanawe.

“Baba mwa mwanangu ni Naseeb Juma Abdul aka Diamond Platinumz. Sababu yangu kusema hivyo ni kuwa simjui baba halisi wa mwanangu. Nimeamua kumpa Diamond mwanangu. Diamond anajua kuwalea watoto na anawapenda pia. Aliniambia nimwarifu nitakapojifungua na kuahidi kukidhi mahitaji yangu ya kila wiki. Nimejifungua na mwana wangu ni wa Naseeb Juma Abdul.” Gigy alisema.

Gigy aliyasema hayo siku chache baada ya kumtema mpenziwe Moj ambaye alimkashifu kwa kuwa na wapenzi wengine na kumdhulumu wakati wa uja uzito wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad