Good News: Wabunge Wachangia Posho Yao kwa Maharusi wa Kihistoria

Mfululizo wa vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeendelea hii leo katika hatua ya maswali na majibu ambapo kwa kauli moja wameadhimia kuchangia sehemu ya posho yao kwaajili ya maharusi wa kihistoria, Jivunie Mbunda na mkewe Bahati Ramadhani waliotembelea Bungeni.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea  kuomba mwongozo wa  Spika wa Bunge ili wabunge waridhie kuchangia Shillingi 20,000 kutoka kwenye posho ya vikao vya leo kwaajili ya kuwachangia maharusi hao.
"Mheshimiwa Spika nilikuwa naomba mwongozo wako kwanini katika posho zetu za leo Wabunge tusikatwe Shillingi elfu 20,000 ili iwe mchango katika kufanikisha ndoa hii ili na wao sasa waweze hata wakaanzie maisha na iwe ni pongezi yetu kwa jambo hili", amesema Mtulia.

Naye Spika wa Bunge, Job Ndugai aliuliza kwa wabunge endapo wanaunga mkono mwongozo huo au la! Ndipo wabunge wakakubali kwa sauti moja na mwongozo ukakubaliwa .

"Kwa kauli moja maharusi mtachangiwa elfu ishirini ishirini kwa kila Mbunge aliyepo humu, hongereni sana na karibuni Bungeni . Hiyo ni zawadi ya wabunge kwenu kwa kutambua jambo hili muhimu sana la upendo wa ajabu ambao mmeufanya, ahsanteni sana na niwashukuru wabunge kwa takrima hii ambayo mmeifanya na Mungu atawalipa", amesema Mhe, Spika.

Jivunie Mbunda ambaye ni mume ana ulemavu ambapo hawezi kumudu kutembea mwenyewe lakini Bahati Ramadhani ambaye ni mke hana ulemavu wowote

Maharusi hao walizua gunzo kubwa  mwezi uliopita baada ya kufunga ndoa katika Wilaya ya Newala mkoani Mtwara

Top Post Ad

Below Post Ad