Hairuhusiwi Polisi Kumchukulia Hatua Mtu kwa Kosa la Mtu Mwingine- Mwigulu Nchemba

Hairuhusiwi Polisi Kumchukulia Hatua Mtu kwa Kosa la Mtu Mwingine- Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amesema si sawa Jeshi la Polisi kumchukulia hatua mtu ambaye si mkosaji kwa kosa la mtu mwingine.

Dk Mwigulu amesema hayo bungeni leo Juni 13, 2018 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Devotha Minja aliyeuliza kumekuwa na tabia mbaya ya jeshi la polisi, wanapokwenda kumkamata mtu, wakimkosa wanamkamata mbadala, mke au mme, je jeshi la polisi wanatoa wapi mamlaka haya kwa kumkamata mtu na kumtesa?

Akijibu swali hilo, Waziri Mwigulu amesema Jeshi la polisi linafanya kazi kwa mujibu wa sheria, hakuna mtu anayeruhusiwa  kuadhibiwa kwa mbadala.

“Kosa linabaki kwa muhusika na kama kuna mtu anaweza kusaidia afanye hivyo lakini si kuchukua adhabu kwa mtu mwingine.”amesema
Chanzo: Mwananchi
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad