Hakuna Mwanamke Yeyote Anayeweza Kunichukulia Mume Wangu Dogo Janja- Irene Uwoya

 Hakuna Mwanamke Yeyote Anayeweza Kunichukulia Mume Wangu Dogo Janja- Irene Uwoya
STAA mkali wa filamu Bongo, Irene Uwoya amefunguka kuwa yeye ni mwa­namke anayejiamini kuliko watu wanavyo­dhani na wala hana wasiwasi na mwan­amke yeyote kum­chukulia mumewe, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Uwoya alisema alipoamua kuingia kwenye ndoa na mwanamuz­iki huyo alijua wazi ‘nyakun­yaku’ wapo, la­kini kikubwa anajiamini.

Akasema hata mumewe huyo aende wapi anajua hawezi kuhangaika na wanawake wen­gine kwa sababu yeye ni mwanamke aliyekamilika.

“Mimi sio mwan­amke wa kufuatana na mume nyuma kwa sababu najiamiani kuliko na ninajua wazi hakuna ambaye anaweza kunin­yakulia mume wan­gu. Najiamini kila idara mimi sina wasiwasi wowote,” alisema Uwoya.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad