BUNGENI, DODOMA: Wabunge wa CHADEMA, Halima Mdee(Kawe) na John Mnyika(Kibamba) wamemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kuwaeleza Watanzania Tsh. Trilioni 1.5 zilizoibuliwa na CAG ziko wapi
Wakizungumza leo Juni 5, wabunge hao wamemtaka CAG kufanya ukaguzi maalumu wa fedha hizo na deni la Taifa huku wakisema kama Dkt. Mpango ameshindwa kuongoza wizara hiyo ni bora akajiuzulu ili asiwe waziri wa fedheha
Halima Mdee naye alipigilia msumari kwa kusema Waziri Mpango anatakiwa ajibu hoja kuhusu Tsh. Trilioni 1.5 na Tsh. Bilioni 200 zilizotajwa kupelekwa Zanzibar ni zipi?
Aidha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amewataka Wabunge kutojadili suala la Trilion 1.5 ndani ya bunge kutoka kwenye ripoti ya CAG hadi kamati ya PAC itapowasilisha ripoti yake