Hatari ya kushiriki ngono kwa njia ya mdomo


Jamii imeshauriwa kutojihusisha kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo kwa sababu usababisha magojwa ikiwemo saratani ya koo na kinywa kwa ujumla


Picha ya ulimi uliyoathirika kutokana na ugonjwa wa ngono

Akizungumza na East Africa Television Dkt Martin Chuwa kutoka Muhimbili amesema kuwa kitendo hiki cha ngono huathiri mfumo wa upumuaji na matokeo yake ni saratani ya koo.

“kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo husababisha virusi vya saratani na upenya katika michubuko na kuingia kwenye chembechembe za fizi kwenye ulimi na kwenda katika njia ya juu ya hewa na vitapenya ndani na kuharibu zile chembe chembe na zitaanza kukua na kusababisha saratan”, amesema Dkt. Martin.

Aidha ameongeza kuwa wengine hufanya kitendo kwa kuiga eti 'fashioni' lakini hawajui madhara yake ni pamoja na kupata magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi.

Hata hivyo Dkt Martin ameongeza kuwa wengine hufanya mapenzi kwa njia ambazo siyo sahihi kwa kupenda lakini wengine hufanya kwa sababu ya utamaduni wao, Mfano baadhi ya makabila nchini ambapo binti akienda kuolewa huchunguzwa kwanza kama ameshashiriki ngono. Kwa hiyo mabinti hao hutumia nafasi hiyo kushiriki ngono kwa njia nyingine ikiwemo ya mdomo.

EATV
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad