Michuano ya Kombe la Dunia imezidi kuelekea patamu ambapo leo jumla ya mechi nne zitakuwa zinawasha viwanja moto nchini Urusi.
Croatia ambao wanaongoza kundi D wakiwa na alama zao 6 kileleni watakuwa wanacheza dhidi ya Iceland kuanzia saa 3 kamili usiku.
Wakati huo Denmark itakuwa inakipiga na Ufaransa kwenye kundi C na mchezo huo ukianza majira ya saa 11 kamili jioni.
Australia nayo itakuwa inacheza dhidi ya Peru kwenye mchezo wa kundi C ambapo mechi hiyo itaanza kupigwa kuanzia saa 11 jioni.
Mechi ambayo inasubiriwa kwa hamu na Waafrika wengi pamoja na wale mashabiki wa Messi ni Nigeria dhidi ya Argentina itakayoanza saa 3 usiku.
Mechi hii inapewa nafasi kubwa ya Messi kuamua hatima ya taifa hilo kama itaweza kupenya dhidi ya Nigeria ambapo njia pekee ya kusalia kwenye mashindano hayo leo ni kupata matokeo ikipaswa kufunga mabao mengi.
Wakati huo Argentina ikipambana kupata matokeo, maombi yao yatakuwa kwenye mchezo baina ya Iceland na Croatia wakihitaji Iceland iweze kupoteza au kwenda sare na wao wapate matokeo ili waweze kufuzu kuingia 16 bora.