Hatimaye Jeshi la Polisi Lamdaka House Girl Aliyemuua Bosi Wake na Kichanga

Hatimaye Jeshi la Polisi Lamdaka House Girl Aliyemuua Bosi Wake na Kichanga
Mfanyakazi wa ndani aliyemuua mwajiri wake pamoja na mtoto wake mwenye miezi mitatu huko Muhoroni, Kisumu nchini Kenya na kutokomea kusikojulikana amekamatwa Uganda na jeshi la polisi la nchi hiyo.

Jacky Auma alikamatwa katika eneo la Namayisi nchini Uganda baada ya jeshi la Polisi nchini Kenya kuwapa taarifa juu ya mtuthumiwa huyo kukimbilia katika mipaka ya nchi hio.

Jacky anatuhumiwa kutenda tukio hilo wiki iliyopita kwa kumpiga mtoto wa mwajiri wake mpaka kufa kisha akamchoma mwajiri wake na kisu mara kadhaa kabla ya kumchoma na kitu kinachodhaniwa kuwa ni pasi ya umeme au tindikali na kumfanya apoteze uhai wake.

Aidha Afisa Polisi wa kituo cha Busia amethibitisha kukamatwa kwa Jacky na amesema kuwa wako wanaandaa utaratibu ili mtuhumiwa huyo arudishwe nchini Kenya akafunguliwe mashitaka.

Top Post Ad

Below Post Ad