"Shaa hayupo sawa Kisaikolojia" - Master J


Mtayarishaji wa Muziki Mkongwe, Joachim Kimaro, Master J ameweka waazi kwamba  kwa sasa mwanamuziki, Malikia wa uswazi, Shaa, hayupo sawa kisaikolojia kutokana na matatizo aliyoyapitia hapo nyuma ikiwa  kumpoteza mama yake mzazi ndiyo maana amekaa kimya kwenye 'game'.


Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ndani ya East Africa Radio, Master J amesema kwamba yeye siyo sababu ya Shaa amaye ni mpenzi wake wa muda mrefu, ila amekubaliana na maamuzi ya msanii huyo kukaa kimya ili kwanza aweze kutuliza akili kwa yale ambayo ameyapitia.

"Yupo very private yule mtu. Watu wengi hawafahamu kama mama yake aliugua kwa muda mrefu na Mungu aishamuita hivyo kwa takribani miaka miwili hayupo sawa. Aliomba time-out. Watu wanadhani ni mimi nambania lakini siyo kweli, ni kwamba hayupo sawa kisaikolojia. la mimi na yeye bado tupo na tunaishi pamoja".

Mbali na hayo Master J ameweka wazi mbali na kuwa Shaa yupo kimya kwenye muziki ndiye mtu ambaye anasimamia biashara zake za kilimo ambazo ameamua kujikita nazo baada ya kuachana na kazi ya utayarishaji wa muziki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad