Hiki Hapa Chanzo cha Mkurugenzi NHC Nehemia Mchechu Kutumbuliwa

Hiki Hapa Chanzo cha Mkurugenzi NHC Nehemia Mchechu Kutumbuliwa
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemia Mchechu.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi(kulia), na aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemia Mchechu.

Kupitia Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Dorothy Mwanyika imesema kuwa kwa mamlaka aliyonayo waziri Lukuvi chini ya kifungu cha 18(1) cha sheria ya Shirika la Nyumba la taifa amesitisha uteuzi huo kuanzia leo Juni 20, 2018.

“Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 18(I) cha sheria ya Shirika la Nyumba la Taifa ya mwaka 1990 pamoja na marekebisho yake mwaka 2005, ametengua uteuzi wa mkurugenzi wa shirika hilo”, imesema Taarifa.

Awali katika taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Disemba 16, 2017 ilimtaka mkurugenzi huyo kusimama majukumu yake ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikimkabiri za utendaji mbovu.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad