Hili Ndilo Kanisa la Walevi la Afrika Kusini Linalotukuza Unywaji Pombe

Hili Ndilo Kanisa la Walevi la Afrika Kusini Linalotukuza Unywaji Pombe
Wakati wa kumuomboleza mwanaharakati aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Winnie Mandela, siku moja, kundi la waumini walioonekana kulewa walizua kionja.

Walikuwa wakilia na kuimba "Mama, Mama". Walijitetea kwamba nao pia walikuwa na haki ya kumuomboleza mtu waliyemuenzi sana.

Hakuwa mwingine ila Papa Makiti kiongozi wa kanisa jipya nchini Afrika Kusini ambalo limekuwa likiwashangaza wengi.

Kanisa hilo linalofahamika kwa jina Gobola (yaani nipe Ulevi ninywe kidogo kwa Lugha ya Kitswana, moja ya lugha rasmi nchini humo) lina mwaka mmoja hivi tangu lianzishwe.

Mwasisi wa kanisa hilo ni Father Tsietsi D Makiti, 53, ambaye kwa sasa anajiita Papa Makiti. Hujieleza kama papa wa kwanza mweusi kutoka bara la Afrika.

Alilianzisha kanisa hilo katika baa moja, na kanisa hilo hufanya ibada zake katika baa na vilabu.

Mhubiri awaomba waumini wamnunulie ndege Marekani
Aliambia mwandishi wetu wa Afrika Kusini Omar Mutasa kwamba kanisa la Gobola na ulevi, vyote ni vya Mungu na ni wajibu wake kuwapa nasaha bora walevi wote waliofukuzwa kwenye makanisa mengine.

Kanisa kuu la Gobola limo ndani ya baa inaitwa Freddie's Tarvern na mwenye baa hiyo Askofu Freddie Mathebula ndiye naibu wa Papa Makiti, husaidia kuongoza mahubiri na ibada wakati mwingine.

Tangu kuanzishwa kwake, kanisa hilo limekuwa likipata umaarufu na inakadiriwa kwamba kwa sasa lina waumini kati ya 500 na 2,000, ingawa idadi yenyewe ni vigumu kuithibitisha.

'Huu ni ukumbi kwa watu kuja pamoja kwa jina la Mungu bila kuaibishwa kwa kuwa walevi," anasema.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad