Hivi Ndivyo Walinzi 12 wa Rais Kim Jong Un Wavyoulinda Msafara Wake Singapore

Hivi Ndivyo Walinzi 12 wa Rais Kim Jong Un  Wavyoulinda Msafara Wake Singapore
Ulimwengu kwa mara nyengine ulipata fursa ya kuwatazama walinzi 12 wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un wakikimbia wakati walipokuwa wakiulinda msafara wake nchini Singapore.

Lakini wana majukumu mengi kwa sababu linapojiri swala la usalama wa kiongozi huyo, taifa la Korea liko tayari kufanya chochote .

Mchanganuzi Michael Madden anaelezea zaidi kuhusu kundi hili la wanaume. Wakati anapokuwa Korea Kaskazini , mlinzi wa karibu wa Kim ana laini tatu tofauti zinazomzunguka.

Walinzi wanaokimbia kandokando ya gari lake aina ya Limousine na wale wanaotembea kwa mguu ni miongoni mwa maafisa wa afisi kwa jina Central Party Office #6, inayojulikana rasmi kuwa afisi ya wapiganaji.

Wao ndio wanaomlinda rais huyo na huchaguliwa kutoka katika jeshi la Korea. Huchaguliwa kutokana na vigezo vya , urefu-wanatakiwa kuwa na urefu sawa na kiongozi wao na wawe wanaweza kuona vizuri.

Wanatakiwa kuwa na uwezo kama vile kupiga risasi na kupigana judo, karate na masumbwi.



Tags

Top Post Ad

Below Post Ad