Hizi Hapa Faida 7 za Kulala Uchi
June 27, 2018
1. Kupata usingizi wa kutosha;* ukilala bila nguo kabisa mwili wako unakua huru sana, nguo hua na tabia ya kukubana sana na kukunyima usingizi wa kutosha kitu ambacho wewe kama mlalaji unaweza usigundue...wakati mwingine huenda umeshawahi kulala umevaa shati lakini asubuhi ukajikuta huna, hii ni kwasababu ukiwa katika nje ya fahamu yaani usingizini uliamka ukavua mwenyewe bila kujua sababu usingizi ulikua haupatikani vizuri.
2. Huzuia magonjwa ya ngozi;* ukilala bila nguo, joto lako la mwili hushuka kidogo na katika hali ya kawaida wadudu nyemelezi wa mwili hutaka sehemu yenye joto au unyevunyevu ili kuweza kushambulia hivyo ukilala bila nguo wadudu hawa hawatapata nafasi ya kuushambulia mwili wako na kukuletea magonjwa,,,hata kipindi cha baridi ni vizuri kujifunika na blanketi nyingi kuliko kuvaa nguo.
3. Husaidia kupunguza uzito;* ukilala na nguo, sababu ya ule usumbufu mtu hupata msongo wa mawazo na hali hiyo husababisha wewe kujisikia njaa na kutaka kula zaidi wakati wa usiku lakini mtu anayelala bila nguo anarelax sana na kusinzia bila hata kusikia dalili za njaa.
4. Hulinda sehemu za siri;* kwa mwanaume kulala bila nguo huweka korodani zako katika hali ya ubaridi na kusaidia kutengeneza mbegu nyingi za kutosha, lakini pia kwa mwanamke huupa uke hewa ya kutosha ya oksijeni na kuzuia magonjwa ya fangasi yanayopenda kushambulia huko.
5. Hunogesha tendo la ndoa na mahusiano;* utafiti unaonyesha kwamba wanandoa wanaolala bila nguo kila siku hushiriki tendo la ndoa mara nyingi zaidi kuliko wale wanaolala na nguo na hii huongeza chachu ya mahusiano na kufanya wajione wapya kila siku sababu ya miili yao kutengeneza homoni ya oxytocin ambayo ni homoni ya upendo.
6. Hupunguza kasi ya kuzeeka;* ukilala bila nguo unatengeneza mazingira mazuri sana ya homoni za mwili wako kufanya kazi sana kuliko kipindi ukilala na nguo ambapo homoni zako zinafanya kazi kwenye mazingira magumu...kifupi ni kwamba kulala na nguo kunakufanya uzeeke haraka.
7. Hukupa furaha na uhuru* ; kwa hali ya kawaida tu mwanamke anapotoka kazini au mizungukoni na kufika nyumbani kitu cha kwanza kabisa kufanya ni kuvua sidiria na kuitupa huko sababu ya kubanwa sana kwa siku nzima, kuvua humpa uhuru sawa sawa na mtu ambaye analala bila nguo ambaye hupata faida hiyo.
*Mwisho* ; chukua hatua sasa, kama ulikua unalala na nguo ni muda wa kuanza kufanya mabadiliko na kumuhusisha mwenzako..
Tags