Hizi Hapa Sifa na Uwezo wa Walinzi 12 wa Kim Jong Un Wanaomlinda Kwa Kukumbia Pembeni ya Gari Kim Jong Un
June 11, 2018
Ulimwengu kwa mara nyengine ulipata fursa ya kuwatazama walinzi 12 wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un wakikimbia wakati walipokuwa wakiulinda msafara wake nchini Singapore.
Lakini wana majukumu mengi kwa sababu linapojiri swala la usalama wa kiongozi huyo, taifa la Korea liko tayari kufanya chochote .
Mchanganuzi Michael Madden anaelezea zaidi kuhusu kundi hili la wanaume. Wakati anapokuwa Korea Kaskazini , mlinzi wa karibu wa Kim ana laini tatu tofauti zinazomzunguka.
Walinzi wanaokimbia kandokando ya gari lake aina ya Limousine na wale wanaotembea kwa mguu ni miongoni mwa maafisa wa afisi kwa jina Central Party Office #6, inayojulikana rasmi kuwa afisi ya wapiganaji.
Wao ndio wanaomlinda rais huyo na huchaguliwa kutoka katika jeshi la Korea. Huchaguliwa kutokana na vigezo vya , urefu-wanatakiwa kuwa na urefu sawa na kiongozi wao na wawe wanaweza kuona vizuri.
Wanatakiwa kuwa na uwezo kama vile kupiga risasi na kupigana judo, karate na masumbwi.Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @BBCLBickerMwisho-mlinzi mmoja huchunguzwa familia yake na vizazo vyake vilivyopita .
Maafisa wengi wa wapiganaji hao wana uhusiano na familia ya Kim Jong Un ama familia kubwa za Korea Kaskazini.
Wanapokubalika kuwa walinzi { huwezi kukataa kazi hiyo} hufanyiwa mafunzo ya kiwango cha juu .Walinzi hao hufunzwa kuwa na ujuzi maalum.
Hufunzwa kwa kutumia bunduki, mbinu za uvamizi, judo, karate , kung fu na taekwndo .
Walinzi hao humzunguka kiongozi hiyo wakimlinda na wanaweza kuona kwa kuzunguka digree 360 kuwatazama watu walio karibu naye na walipo.
Wanaotembea , mbele yake ni kati ya walinzi watatu hadi watano akiwemo mkurugenzi wa agfisia hiyo ya wapiganaji.
Pamoja naye , ni walinzi wanne hadi sita , wawili ama watatu wakiwa upande wake wa kulia .
Kuna wengine wanne ama watano nyuma yake.
Ili kuonyesha uwezo wao katika utawala huo, ndio raia pekee wanaokubaliwa kubeba bunduki zilizo na risasi karibu na kiongozi wa taifa lao, sana sana huwa bunduki zinazodaiwa kuwa automatic pamoja na silaha nyengine.
Walinzi hao walioonekana wakikimbia kandokando ya msafara wa rais Kim wakati mkutano wa mataifa ya Koreamwezi Aprili
Licha ya kubeba silaha, ulinzi mkubwa wanaompatia rais Kim jong un ni ujuzi walio nao katika kuwachunguza watu walio karibu na kiongozi huyo na kukabiliana na tishio lolote kwa kutumia mikono yao na mwili.
Wakati Kim Jong il alipokuwa hai mlinzi mmoja alikuwa akiwalinda maafisa wakuu wawili anaondamana nao.
Walinzi wa Kim Jong Un ikilinganishwa na wale wa babake ni wachache na hawaonekani mara kwa mara. Walinzi hao huvalia suti za magharibi kama wanavyoonekana nchini Singapore .
Dereva wa Kim Jong un huvalia glavu za plastiki ama za ngozi kushika usukani. Pia hutumia mawasiliano ya redio kupitia hedifoni.
Hatahivyo mbinu zao za mawasiliano ni za zamani.
Kitengo hicho cha afisi ya wapiganaji kina takriban kati ya maafisa 200-300, ambao nusu yao ni walinzi na waliosalia ni madereva na wafanyikazi wa kiufundi.
Huku baadhi ya walinzi wa viongozi hao wakiwa watu walio na uzoefu mkubwa , wengi wao huwa wamefanya kazi kwa miaka 10.