Hotel yaamuriwa kumlipa zaidi ya Milioni 68 Mwanamke waliyemuita ‘Kahaba’

Leo June 7, 2018 Mahakama Kuu imeamuru mwanamke aliyetimuliwa katika hoteli moja ya kifahari kwa kudaiwa kuwa kahaba alipwe fidia ya dola 30,000 za Marekani ambazo ni zaidi Milioni 68 za Kitanzania katika Mahakama kuu ya Kenya iliyopo Nairobi.

Jaji Msagha aliitaka hoteli ya Intercontinental kulipa fidia ya milioni 2 na mwanasheria mkuu wa serikali milioni 1 kwa Winfred Clarke kwa kumdunisha na kumharibia jina.

Tukio hilo lilitokea miongo miwili iliyopita mwanamke huyo alipofika hotelini kwa nia ya kufurahia kinywaji akiwa na rafiki yake kabla ya kusimamishwa na mlinzi wa hoteli kwa sababu hakuwa ameandamana na mwanaume.

Clarke hata hivyo, alienda hadi eneo la kuuzia vileo ambapo aliagiza bia mbili kabla ya kulazimishwa kulipa “ada ya kujisitiri” ambayo hakuelewa ni kwa nini alitakiwa kulipa.

Baadaye, alitolewa kwa nguvu kutoka hotelini humo na kuzuiwa kukaa eneo ambalo wageni wanakaa wanapongojea teksi, kabla ya polisi kuitwa na kumkamata ambapo alizuiliwa kwa siku mbili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad