Huddah Monroe Akata Shauri Aamua Kuasili Mtoto Badala ya Kuzaa

Huddah Monroe ‘The Boss Chick’ BAADA ya kukaa muda mrefu bila kupata mtoto, muuza nyago kwenye mitandao na mjasiriamali, Huddah Monroe ‘The Boss Chick’ ametimiza ndoto zake za kuasili mtoto wa kike.

Huddah ambaye alikuwa Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita katika Sikukuu ya Idd Pili alisema kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akipenda watoto wadogo kutokana na maisha aliyopitia na alikuwa akitaka kutimiza ndoto zake kwa kuasili.

“Nimeasili mtoto kwa sababu mara nyingi najihisi kama wao. Wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumlipia ada. Nilimuuliza unataka kwenda shule? Niliona ana ndoto, ni kweli alikuwa akihitaji kwenda shule. Nikamchukua, bado yupo na mama yake lakini namlipia kila kitu, napenda watoto,” alisema Huddah.

 NAIROBI, Kenya

GPL

Top Post Ad

Below Post Ad