Idadi ya Vifo Ajali ya Wanafunzi UDSM Yaongezeka ...... Majeruhi Aliyekuwa Akipatiwa Matibabu MOI Afariki

 Idadi ya Vifo Ajali ya Wanafunzi UDSM Yaongezeka ...... Majeruhi Aliyekuwa Akipatiwa Matibabu MOI Afariki
Majeruhi mmoja kati ya wawili wa ajali iliyotokea eneo la River Side jijini Dar es Salaam ikihusisha gari la wagonjwa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amefariki dunia leo Juni 12, 2018.


Majeruhi huyo alikuwa akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (Moi) baada ya ajali iliyotokea usiku wa jana Juni 11, 2018.

Ofisa uhusiano wa Moi, Patrick Mvungi amesema waliwapokea majeruhi hao saa 9:30 usiku wakitokea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amewataja majeruhi hao kuwa ni Abishai Nkiku (24), mwanafunzi wa UDSM na Jonathan Lugando (40), mhudumu wa chuo hicho.

"Madaktari wanaendelea kumhudumia Nkiku ingawa ameumia sana kichwani,” amesema Mvungi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Daruso waliofariki awali katika ajali hiyo ni Maria Gordian ambaye alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza na Steven Sango wa wa mwaka wa pili.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad