Ifahamu Sababu ya Mwanamuziki Amani wa Kenya Kuamua Kufanya Muziki wa “Gospel”

Ipate hii story kutoka kwa staa wa muziki kutokea +254 Nairobi Kenya Ceciliah Wairimu maarufu kama Amani ambaye miaka kadhaa iliyoipita alitamba na ngoma zake kali ikiwemo Missing my baby, Tonight na kiboko yangu ambazo zilimpatia umaarufu Afrika Mashariki.

Staa huyo ameonekana kuachia ngazi za muziki wa kidunia na kuamua kumrudia Mungu kwa kufanya muziki wa gospel na ame’share mawazo yake na maisha yake mapya na mwandishi wa Daily Nation Lilys Njeru.

Kupitia mahojiano yao Amani ameeleza kuwa kuimba gospel ni kitu ambacho alikuwa akikifikiria kwa muda mrefu na kufikia hatua ya kuchoka kufanya shows usiku na kurudi nyumbani mida ya usiku akiwa amechoka.

“Nimekuwa nikifikiria hichi kitu tokea 2011 lakini niliendelea kufanya muziki wangu wa kawaida, baada ya miaka mitatu iliyopita niliamua kuachana na muziki niliokuwa nikifanya”
 "Mama yangu ni mtu wa kwanza kufahamu kuhusiana na mimi kuachana na muziki wa kidunia na kufanya gospel na alifurahi sana kwasababu amekuwa akinipa ushirikiano sana”

Tazama Rosa Ree na Emtee Walivyokinukisha Kwenye Chupa Hili..Bonyeza Play

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad