IGP Sirro asifu hali ya usalama iliyopo nchini


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewahakikishia wananchi wa Tanzania kuwa hali ya usalama nchini umeimarika huku akiwaonya baadhi ya watu ambao bado wana mdudu wa kichwa juu ya uhalifu waache mara moja kwani Jeshi la Polisi litawashughulikia kwa mujibu wa sheria. 

IGP Sirro ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Drive kilichorushwa na East Africa Radio hivi karibuni na kusema Jeshi lake lipo imara katika kuhakikisha hali ya usalama wa raia na mali zao katika sehemu zote. 

"Hali ya Kibiti hadi hivi sasa ni shwari kabisa na juzi kulikuwepo na mashindano ya Sirro CUP baada ya ile ngoma kuwa imekwenda vizuri na wale waliotandikwa kwa mujibu wa sheria wamekimbia wengine wamepelekwa Mahakamani na wapo waliotangulia mbele za haki 'kufa'. Sasa hivi hali ni shwari sana", amesema IGP Sirro. 

Pamoja na hayo, IGP Sirro ameendelea kwa kusema "ni wape salamu wale watu ambao bado wanao huyu mdudu anayezunguka kichwani mwao ambao wamebakia wachache wasithubutu tena kurudi Tanzania kufanya yale ambayo walipanga kuyafanya. Tutawagonga sana na sheria itachukua mkondo wake na wasije wakailaumu serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad