Irani Yaingia Katika Historia Yawaruhusu Wanawake Kuingia Uwanjani kwa Mara ya Kwanza

Irani Yaingia Katika Historia Yawaruhusu Wanawake Kuingia Uwanjani kwa Mara ya Kwanza
Taifa la Iran June 20 2018 limeingia katika historia mpya katika michuano ya Kombe la Dunia 2018 inayoendelea nchini Urusi baada ya kuruhusu mashabiki wake wa kike waingie uwanjani kwenda kuishangilia timu yao ikicheza dhidi ya Hispania.

Iran ambao hadi wanaingia katika uwanja wa Azadi jijini Tehran kucheza dhidi ya Hispania walikuwa na point tatu, wameambulia kipigo cha goli 1-0, goli pekee la Hispania lilifungwa na Diego Costa dakika ya 54, pamoja na Iran kuongeza nguvu ya mashabiki wake wa kike uwanjani lakini haikusaidia.



Kama ufahamu tu nchi ya Iran imeruhusu mashabiki wake wa kike kuingia uwanjani kutazama mpira kwa mara ya kwanza June 20 baada ya miaka 37 toka tukio kama hilo litokee 1979, Iran ni miongoni mwa baadhi ya nchi za kiharabu ambazo haziruhusu wanawake kwenda uwanjani.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad