Jaji Mutungi Avionya Vyama vya Siasa

Jaji Mutungi  Avionya Vyama vya Siasa
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa na wanachama wake kutekeleza majukumu yao ya kisiasa kwa kufuata na kuzingatia sheria na Kanuni za vyama vya siasa na sio vinginevyo.


Jaji Mutungi ametoa kauli hiyo leo Juni 20, 2018 kufuatia tabia iliyojitokeza ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini kutumia vibaya vyombo vya habari, hususani mitandao ya kijamii kufanya vitendo au kutoa kauli ambazo zinavunja sheria za nchi na ni wito wangu kwao kuacha tabia hiyo mara moja.

"Ninasisitiza kuwa viongozi wa vyama vya siasa wasitumie vibaya dhana ya demokrasia na uhuru wa habari, kuvunja Sheria za nchi. Ieleweke kwamba mtu yeyote anapokiuka sheria za nchi, Sheria itachukua mkondo wake bila kujali wadhifa wa mhusika katika chama cha siasa", amesema Jaji Mutungi.

Kwa upande mwingine, Jaji Mutungi ametoa rai kwa viongozi wote wa vyama vya siasa na wanachama wote wa vyama vya siasa nchini kuheshimu sheria za nchi wakati wote ili kudumisha na kukuza demokrasia ya vyama vingi nchini.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad