Jay-Z ashtakiwa kwa kutomlipa Prodyuza


PRODYUZA wa muziki, Raynard Herbert, wa Marekani amefungua mashitaka dhidi ya  mwanamuziki Jay-Z wa Marekani kwa kutomlipa asilimia moja ya mauzo ya albam yake ya “Reasonable Doubt” kama walivyoahidiana. 

Herbet amesema alitumia juhudi zake kuiuza albamu hiyo mwaka 1995 lakini miaka 10 sasa imepita tangu Jay-Z asimamishe malipo ya fedha hiyo. 

Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, kila kitu kilikuwa kinakwenda vizuri hadi Novemba 2008, mfanyabiashara huyo alipoacha kulipwa. 

Amesema mnamo Mei 2010 alijaribu kufuatilia malipo yake hayo lakini hakufanikiwa chochote, hivyo hivi sasa anafuatilia ili apate chake pamoja na riba zinazotokana na mchakato huo. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad