Mtaalam wa maswala ya ngono nchini Kenya Maurice Matheka amepinga dhana kwamba misimu ya baridi huchochea kuzaliwa kwa watoto wengi.
Katika mahojiano na BBCswahili, mtaalam huyo anasema kwamba fikra hiyo imetumiwa na wanaume kama chambo cha kuwavutia wanawake katika mazungumzo wakati wa msimu wa baradi.
Matheka anasema kuwa Waafrika wamelelewa katika tamaduni ambazo zinawafanya kuhisi kana kwamba mkutano wowote wa mume na mke katika eneo la faragha huchochea kufanyika kwa mapenzi.
''Ni kweli kwamba misimu ya baridi huwachochea wanaume na wanawake kukumbatiana ,lakini swala kwamba hatua hiyo inaweza kuchochea ngono sio la kweli. Wenzetu wazungu kwa mfano wana misimu ya baridi lakini hilo halitokei'', alisema mtaalamu huyo.
''Msimu wa baridi humuathiri mwanamume na hivyobasi yeye hutaka joto mwilini lakini sio kwamba watu wanapokumbatiana husababisha kufanyika kwa tendo la ngono''.
Kulingana na mwanasayansi huyo, matokeo yalibaini kwamba wanafunzi waliotekeleza ngono chini ya mara moja kwa wiki walikuwa na kiwango cha juu cha kinga ikilinganishwa na wale ambao hawakushiriki kabisa.