NAIROBI, KENYA: Watu watatu wamethibitika kupoteza maisha huku saba wakiokolewa kufuatia kuanguka kwa jengo la ghorofa 5 asubuhi ya leo Juni 03, huko Huruma Nairobi
Naibu Mkuruguenzi wa Kitengo cha kupambana na majanga, Pius Masai, amesema mtu mmoja alikutwa amefariki kwenye kifusi huku wawili walifariki wakipelekwa hospitali. Watu watatu wamefikishwa hospitalini na wanapatiwa matibabu
Masai ameeleza kuwa wapangaji wengi wa jengo hilo waliondoka baada ya jengo hilo kutengeneza nyufa kubwa muda mfupi kabla ya saa sita usiku, siku ya Jumamosi kumakia Jumapili
Taratibu za uokoajia bado zinaendela ambapo wananchi walipo katika majengo ya jirani wameondolewa baada ya wakoaji kusema eneo hilo si salama kwa kuwa inawabidi kubomoa majengo kadhaa ili kulifikia jengo lililoanguka
Naibu Kamishina wa Kaunti ndogo ya Mathare, Patrick Mwangi amesema jengo lililoanguka lilikuwa limewekewa alama ya kubomolewa lakini wapangaji waliingia kinyemela na kuendelea kuishi humo kwa miezi kadhaa