Jeshi la Polisi Lamshikilia Mwanaume Aliyemuua Mhadhiri wa UDOM

Jeshi la Polisi Lamshikilia Mwanaume Aliyemuua Mhadhiri wa UDOM
JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia mtuhumiwa wa mauaji a;liyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Rose Manfredy Mndenye ( 31) aliyedaiwa kuuawa na mume wake kwa kile kinachosemekana kuwa ni sababu za wivu wa mapenzi.



Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma, leo Jumatatu, Juni 18, 2018, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema Jeshi hilo limefanya uchunguzi na kubaini mtuhumiwa huyo alikuwa amejificjha mkoani Morogoro, hivyo likafanya jitihada za kumnasa na kumtia mikononi mwa dola.






“Baada ya uchunguzi tuliofanya, tumemkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Mhadhiri wa (UDOM), marehemu Rose Manlfred Mdenye aliyeawa kwa kukatwa katwa na visu na mtu anayedaiwa kuwa ni mume wake eneo la Swaswa mtaa wa Sarungai.



“Tumemkamata akiwa amejificha katika Kijiji cha Chiwachiwa, Kata ya Mbingu wilayani Ifakara mkoani Morogoro, na sasa mtuhumiwa yupo sero, tunaendelea na uchunguzi zaidi na tukikamilisha tu tutamfikisha mahakamani.



Tukio la kuuawa kwa Rose liliyokea Maei 25, mwaka huu majira ya usiku baada ya mumewe huyo kudaiwa kumcharanga visu sehemu mbalimbali za mwili kisha kutokomea kusikojulikana.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad