Jiji la Mwanza Kitovu cha Pili cha Uchumi Tanzania


Na James Timber, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema Jiji lake ni kitovu cha pili cha uchumi ukitoka Mkoa wa Dar es salaam unaochangia mfuko wa taifa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki ya Ecobank  jijini hapa Mongella alisema, zaidi ya shilingi Billion 4 zimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi wa eneo la Fella Wilayani Misungwi lenye ukubwa wa hekta 1500 eneo hilo litajengwa bandari ya nchi kavu ambayo reli ya standard gauge itaishia.

Mongella aliitaka Benki hiyo kutengeneza bidhaa itayoitambulisha kanda ya ziwa na kuwataka wawekezaji wengine waje Mwanza kwa kuwa ujenzi wa viwanda unaendelea na halmashauri zote zinaendelea kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Ecobank Peter Machunde aliwataka watu wanaosambaza maneno ya kuwa benki hiyo ni yakinaijeria waache kwakuwa hiyo siyo benki ya kinaijeria na kuwa Makao Makuu yake ni Togo.

Aidha alisema kuwa benki ya kiafrika (Pan Africa) na sio kama wanavosema baadhi ya watu kuwa ni ya kinaijeria”alisema Machunde.

Pia alisena kuwa Benki ya EcoBank inafanya kazi kwenye nchi 35, ina matawi 1700 na matawi yaliyopo nchini ni matawi saba pekee.

 Tazama Rosa Ree na Emtee Walivyokinukisha Kwenye Chupa Hili..Bonyeza Play


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad