Kumekuwa na taarifa katika mitandao ya kijamii, zinazodai kuwa msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu anaumwa na kudai kuwa ndio chanzo cha ukimya wake katika mitandao na matukio mbalimbali.
Eatv ilimtafuta Wema Sepetu ili kutaka kufahamu ukweli kuhusiana na taarifa hizo lakini hakupokea simu na alivyotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi, amejibu kuwa “Sifanyi interview sasa hivi I’m sorry”.
Meneja wa mwanadada huyo ambaye ni Martin Kadinda, amekanusha taarifa hizo wakati akizungumza na eatv.tv ambapo amedai kuwa Wema kwa sasa uhusiano wake alionao unamfanya kuwa msiri sana kwenye maisha yake ya kawaida.
“Wema Sepetu sio mgonjwa kama taarifa zinavyosambazwa na ukimya wake unatokana na uhusiano wake wa sasa una mbana sana kutokuweka maisha yake hadharani”, amesema Martin.
Hivi karibuni Mama mzazi wa kuwa mwanadada huyo, aliiambia Mahakama kuwa mwanae alikwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibu, kutokana na kushindwa kuhudhuria mahakamani katika kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya.