Kagame Cup Kuzinduliwa Rasmi Kesho

Kagame Cup Kuzinduliwa Rasmi Kesho
Michuano ya Kombe la Kagame inatarajia kuzinduliwa rasmi kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Michuano hiyo ambayo inashirikisha klabu kutoka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambazo ni  12.

Tanzania imewakilishwa na timu nne ambazo ni Simba, Singida United na Azam FC za Tanzania Bara pamoja na JKU ya Zanzibar.

Katika uzinduzi huo Uwanja wa Azam, timu za JKU na Vipers SC zitafungua dimba katika mechi itakayochezwa saa 8.00 mchana na saa 10.00, Azam itaikaribisha Kator FC ya Sudan Kusini.

Pia, saa 11.00 jioni, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, utapigwa mchezo kati ya Singida United na APR Rwanda.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad