Kamanda Muslimu Afunguka Chanzo cha Ajari ya Askari wa JWTZ

Kamanda Muslimu Afunguka Chanzo cha Ajari ya Askari wa JWTZ
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Fortunatus Muslim ametembelea eneo ambalo askari wa JKT walipatia ajali na kubainisha kuwa gari walilotumia halikukaguliwa na polisi hivyo halikuwa na vigezo vya kusafiri umbali mrefu.


Kamanda Muslim mapema leo ametembelea eneo la Mwansekwa ambalo ndio lilisababisha vifo vya askari 12 akiwe mmoja wa Jwtz na Jkt kutokana na mteremko mkali uliopo maeneo hayo na kuahidi kuwachukulia hatua waliohusika na uzembe huo.

“Gari hilo halikukaguliwa na Polisi na hatua kali zitachukuliwa kwa kila aliyehusika na ukodishwaji wa gari hilo”, amesema Kamanda Muslim.

 Kamanda yupo mkoani Mbeya, amabpo alitembelea pia majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda na kusema kuwa miili ya marehemu inatarajiwa kuagwa siku ya Jumanne.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad