Kamati Maalumu Ya Bunge Yaibua Madudu, Mawaziri Watajwa


Kamati iliyoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuchunguza mwenendo wa biashara ya sekta ya gesi asilia nchini imebaini madudu katika sekta hiyo ikiwamo mikataba ya serikali na wawekezaji ilivyoliingiza hasara taifa kupitia sekta hiyo huku mfanyakazi mmoja akilipwa mamilioni.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo iliyoundwa Novemba mwaka jana, Dunstan Kitandula amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo wakati akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo kwa Bunge.

Katika ripoti hiyo, Kitandula amewataja mawaziri zamani wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, Daniel Yona, Nazir Karamagi, William Ngeleja na marehemu Abdallah Kigoda kuingia mikataba hiyo, ambayo alisema imekuwa ikiliingizia hasara taifa.

“Mawaziri hao walikuwa wakisaini mikataba hiyo na makampuni ya kigeni kupitia aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Yona Kilaghani.

“Aidha, katika uchunguzi wetu, kamati ilibaini mfanyakazi mmoja wa kigeni wa Kampuni ya Payet, analipwa mshahara wa Sh milioni 96 kwa mwezi tofauti na wazawa ambao wanalipwa mshahara kidogo.

“Kutokana na hali hiyo, kamati inapendekeza vyombo vya dola vichunguze mikataba yote katika sekta ya gesi iliyoingiwa na viongozi hao ili kuona kama walikuwa na nia njema au waliiisaini kwa kujali maslahi yao,” amesema Kitandula.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad