Kambi ya Upinzani yaitaka KKKT, Kanisa Katoliki kutoijibu serikali


Kambi ya Upinzani Bungeni, imewataka viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Kanisa Katoliki, kutoijibu serikali kuhusu barua waliyopewa na Msajili wa Vyama ya kukanusha waraka wao.

Leo June 06, 2018 Jijini Dodoma Mbunge wa Vunjo, James Mbatia akizugumza na waandishi wa habari kwa niaba ya kambi hiyo amesema mamlaka za nyaraka za makanisa hayo ni mamlaka ya kibiblia.

Amesema makanisa hayo makubwa nchini yamekuwa yakitoa huduma kubwa katika jamii hivyo kwa jambo lililofanywa na msajili wa vyama kisaikolojia wamedharauliwa.

“Sisi tunawashauri viongozi hawa wa dini kutowajibu serikali halafu tuone wanachukua hatua gani,” amesema.

Kwa upande wake Mbunge wa Kibamba, John Mnyika amesema serikali inapaswa kukanusha barua hiyo na kwamba jambo hilo halitakwisha watatumia kanuni za bunge ndani siku 10 kuomba miongozo hadi pale serikali itakapotoa majibu.

Hapo awali Bungue Mbatia alihoji suala hilo wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Hata hivyo Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alimkia kifua Waziri Mkuu akisema kwamba itakumbukwa kuwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea alihoji kuhusu masuala ya dini lakini Spika Job Ndugai akamwambia waziri mkuu hawezi kujibu masuala ya imani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad