Kufuatia kauli hiyo inayotrendi mitandaoni, baadhi ya wadau wamehoji iwapo dini anayoisema inamruhusu kuzaa watoto wanne nje ya ndoa na kila mmoja akawa na mama yake, au ina mruhusu kufanya sanaa ya muziki, kutembea na wanawake na kuwaacha na mambo mengine mengi ambayo yameendelea kuibuliwa mitandaoni kufuatia kauli yake hiyo.
Akizungumzia jambo hilo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyik jana Juni 7, 2018 jijini Dar es salaam, Alikiba alisema kuwa sababu kubwa ya kutoposti picha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo amedai kuwa kufanya hivyo ni kinyume na dini yake ya kiislamu.
Ni kweli Dini yako hairuhusu kumpost marehemu, lakini pia Dini yako hairuhusu uzinifu, dini yako hairuhusu muziki, dini yako hairuhusu kuzaa nje ya ndoa
ReplyDelete