Baada ya Cristiano Ronaldo kutupia ‘hat-trick’ na kuisaidia timu yake ya taifa ya Ureno kutoka sare ya mabao 3 – 3 dhidi ya Hispania hapo jana usiku kwenye michuano ya kombe la Dunia meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa mshambuliaji huyo ni mchezaji ambaye yupo kwa mechi maalum.
Mchezaji huyo bora duniani, Ronaldo amefanikiwa kufunga ‘hat-trick’ za kwanza kwenye michuano hiyo ikiwemo bao lake la ‘free-kick’ na kuisaidia Ureno kupata alama moja kwenye mchezo huo wa ufunguzi wa kundi B.
Mourinho ambaye pia ni raia wa Ureno alishawahi kumfundisha Ronaldo wakati akiwa kocha ndani ya klabu ya Real Madrid hivyo anamfahamu vilivyo uwezo wake ndani ya uwanja.
Akiwa huko nchini Urusi Mourinho amesema kuwa “Anafahamu hilo na kwakuwa anafahamu ndiyo sababu ninavutiwa na baadhi ya wachezaji mfano wake,” amesema Mourinho kupitia Russia Today.
“Kuna wachezaji wapo kwaajili ya baadhi ya mechi, wengine wapo kwaajili ya kila mechi na kuna wachezaji wao wapo kwaajili ya mechi maalum. Wachezaji ambao wapo kwaajili ya mechi maalum yupo mmoja tu.”
“Bao lake la ‘free-kick’ si bora sana ukilinginisha na alicho kifanya Manchester United na alipo jiunga Real Madrid kwa mwaka wake wa kwanza.