Kauli ya Ridhiwani Baada ya Kutembelea Ofisi Yake Iliyoteketea kwa Moto

Kauli ya Ridhiwani Baada ya Kutembelea Ofisi Yake Iliyoteketea kwa Moto
KUFUATIA Jengo la Ofisi yake kuteketea kwa moto juzi Jumapili jioni, Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, leo Jumanne, Juni 19, 2018 amefika katika eneo hilo na kujionea hali halisi ilivyokuwa baadaya ajali hiyo mbaya kutokea.


Ridhiwani ameeleza masikitiko yake kutokana na kuunguliwa ofisi zake hizo huku akisema jambo hilo ni mipango ya Mungu hivyo ni lazima kukubariana na hali halisi.



Mbunge huyo amesema; “Nimefika kwenye eneo la Ofisi ya Mbunge iliyoungua. Nimeona jengo lilivyoharibika. Mungu ameumba mitihani na tujifunze kuikabiri.#ChalinzeNiKaziTu.”




Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Marian Joakim (52) mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika kuchoma ofisi hizo ambapo moto huo uliteketeza vitu vingi na vichache ndivyo vilivyookolewa.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jonathan Shana amesema tukio hilo ni la Juni 17 saa 12 jioni eneo la Bwiringu Chalinze wilaya ya Bagamoyo.

“Mtuhumiwa anadaiwa alikuwa akichoma majani jirani na ofisi hiyo ya mbunge na ukashika moto baada ya kumzidi,mtuhumiwa anashikiliwa kwa mahojiano zaidi. Thamani ya mali zilizoungua haijafahamika ambapo jengo hilo limeteketea kabisa kwa moto huo,” amesema Shana.

Top Post Ad

Below Post Ad