Kenya waanza mchakato wa kumtafuta Rais wa Kwanza Mwanamke

Huku juhudi za kisiasa pamoja na zile za kisheria kuleta usawa wa kijinsia kupitia kuwa na wanawake wengi katika nyadhfa za juu zikiendelea duniani, kipindi kimoja cha runinga kimeanza nchini Kenya kikiwa na lengo la kuendeleza mjadala huo mbele, kupitia ajenda ya 'wanawake kama viongozi' kwa lengo la kukuza usawa wa kijinsia na viongozi wanawake.

Kipindi hicho kwa jina Bi rais chenye sehemu 26 kinatokana na msururu wa kipindi kama hicho nchini Palestina kwa jina Rais ambacho kilikuwa kikishirikisha kumchagua kijana mmoja wa Palestina kuongoza taifa hilo.

Kitatayarishwa na Media Focus on Africa kupitia ufadhili wa Muungano wa Ulaya na kitashirikisha wanawake wenye vipaji vya uongozi kwa lengo la kuongeza uwezo wao kuchukua nyadhfa mbalimbali za uongozi nchini humo.
''Hatutafuti malkia wa urembo, tunatafuta wanawake ambao ni viongozi''. Sio kuwaleta wanawake katika runinga bali kuwafunza na kuwashauri'', alisema afisa wa mradi huo katika Media Focus on Africa Frenny Jowi.

Watakaofuzu watapewa mafunzi ya uongoizi na ushauri ikiwa ni pamoja na mpango wa kuleta amani utakaoonyesha kwamba wanawake wanaweza kuchukua jukumu la kuzuia kuenea kwa uchochezi wa ghasia.

Wanawake walio kati ya umri wa miaka 20 hadi 70 waliomaliza kidato cha nne , wana hadi mwezi Julai 27 kutuma maombi yao ambayo yatatamatishwa kupitia kupatikana kwa Bi Rais wa Kenya.
''Mwanamke atakayefaulu kushiriki katika kipindi hiki atakuwa mfano wetu sote.Tungependa kufanya kazi na wanawake wote watakaotuma maombi yao katika kipindi hicho kama wizara ya Jinsia'', alisema Lydia Mathia mshauri wa waziri wa Huduma kwa umma ,vijana na Jinsia.
Licha ya kuwa na sheria nzuri zinazotoa fursa ya usawa wa uwakilishi wa wanawake, vijana, walemavu na walio wachache, Kenya bado imesalia nyuma ikilinganishwa na mataifa mengine ya bara Afrika katika kuwa na wanawake katika nyadhfa mbali mbali za uongozi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad