Kiboko Azua Taharuki Baada ya Kuonekana Kihonda, Morogoro

Kiboko Azua Taharuki Baada ya Kuonekana Kihonda, Morogoro
Kiboko ameonekana leo asubuhi eneo la kata ya Kihonda, manispaa ya Morogoro barabara kuu ya Dodoma-Morogoro.

MCL Digital ilifika eneo la tukio na kushuhudia kiboko huyo akiwa kajificha chini ya kalavati lenye maji.

Awali, wanafunzi wa darasa la saba waliokuwa wakielekea shule ndiyo walikuwa wa kwanza kumuona kiboko huyo akiwa kwenye barabara ya lami eneo hilo.

Baadaye alitoka barabarani na kuingia kwenye kalavati la maji.

Ilionekana kama umati wa watu uliokuwa katika eneo hilo ulimtia hasira kiboko huyo ambaye alikuwa akitoka na kuingia kwenye maji.
Chanzo: Mwananchi
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad