Kifaa cha Kuwafichua Waongo Chatua kwa Kenyatta
0
June 02, 2018
NA FATUMA MUNA
Maafisa wakuu wa serikali ya Kenya watalazimika kupimwa kwa kutumia kifaa cha kuwafichua watu waongo ikiwa ni miongoni mwa harakati za kukabiliana na ufisadi.
Akihutubia makundi ya raia waliokutana kusherehekea miaka 55 tangu Kenya ijipatie Uhuru , amesema kuwa Kenya italazimika kuangamiza ufisadi kabla ya jinamizi hilo kuangamiza ufanisi na siku za usoni za vizazi vijavyo.
''Wacha nitaje mpango mmoja ambao tunapanga kuidhinisha kukabiliana na ufisadi. Kama hatua ya kwanza , wakuu wote wa idara za kutoa zabuni na zile za hesabu katika wizara za serikali watafanyiwa ukaguzi mpya ikiwemo kupimwa na kifaa cha kuwatambua watu waongo ili kujua maadili yao. Wale watakaofeli watasimamishwa kazi'' amesema.
Kenyatta ameeleza kuwa kifaa hicho ambacho kitafichua maadili ya wafanyakazi ni miongoni mwa mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo.
Hata hivyo hotuba ya rais Kenyatta ni jaribio la kukabiliana na tatizo hilo ambalo kwa limekomaa baada ya kufichuliwa kwamba kiasi cha dola bilioni 8 za Kenya zilipotea katika kitengo kimoja cha serikali takribani wafanyakazi 40 wa umma wanakabiliwa na kashfa hiyo.
Kashfa hiyo ya ufisadi , ambayo ilifichuliwa na wauzaji bidhaa ambao walikuwa hawajalipwa , ilipelekea kuibiwa kwa fedha hizo katika shirika la vijana wa huduma kwa jamii NYS kupitia vyeti bandia na malipo ya ziada.
Tags