“Kigoma Mpo nje ya Tanzania Mpo Porini Sana Mmetengwa”- Msigwa

Mbunge wa Iringa mjini (CHADEMA) mchungaji Peter Msigwa, amesema kuwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma wamesahaulika na Serikali ni kama wapo nje ya Tanzania kutokana na ubovu wa barabara ya Nyakanazi

Msigwa amesema hayo leo Juni 4, 2018 Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kuchangia hoja mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango katika mwaka wa Fedha 2018/2019 na kudai kuwa wabunge wanapaswa kuungana pamoja kuishinikiza Serikali ijenge barabara hiyo.

“Kuhusiana na barabara ya Nyakanazi, tangu nimekuwa Mbunge kipindi cha kwanza nimekuwa nikisikia Kigoma Nyakanazi, kwakweli watu wa Kigoma mnaonewa inabidi tuwasaidie, mpigiwe debe kwakweli mpo porini sana mmetengwa, mimi ilikuwa mara ya kwanza kufika Kigoma kwakweli mpo nje ya Tanzania” amesema Msigwa.

Kwa upande mwingine Mbunge huyo amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imejikita zaidi katika masuala ya fedha na kusahau kujihusisha na mipango kwasababu mipango mingi inayotekelezwa ipo nje ya mpango wa miaka mitano wa Taifa hivyo kushindwa kutekeleza vipaumbele vya maendeleo ya nchi.

Leo Juni 4, 2018 Bunge linajadili Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango katika mwaka wa fedha 2018/2019 na Waziri husika Dkt. Philip Mpango ameomba Bunge kuizinisha jumla shilingi trilioni 12.5 ambapo trilioni 10.07 ni katika matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.2 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad