Rais wa Sudan kusini Salva Kiir na Kiongozi wa waasi Riek Machar wanatarajiwa kutia saini makubaliano waliyoyafanya siku ya Jumatatu, kufikisha mwisho miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenye nchini humo.
Wawili hao walikutana siku ya Jumatatu mjini Khartoum ambapo walifanya mazungumzo na kukubaliana baadhi ya maeneo.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Sudan Al-Dirdiri Mohamed Ahmed amesema maeneo yaliyofikiwa makubaliano yatatangazwa baadaye leo, viongozi hao watakapokutana.
Kiir na Machar Kutiliana Mkataba wa Makubaliano ya Amani
June 27, 2018
Tags