Kijana Nchini Kenya Aishtaki Hospitali kwa Kutumia Nyeti Zake Kinyume na Matwakwa Yake

Kijana Nchini Kenya Aishtaki Hospitali kwa Kutumia Nyeti Zake Kinyume na Matwakwa Yake
Mwanaume mmoja nchini Kenya ameishtaki hospitali ya Agha Khan kwa kutumia nyeti zake kuwafundishia wanafunzi wa kike wanaosoma udaktari kinyume na matakwa yake.

Mwanaume huyo ambaye alipenda kutambulika kama DK kwa ajili ya kutunza faragha yake ,amesema kuwa alienda katika hospitali hiyo kama mgonjwa kumuona Dokta Samnakay na sio kutumika kama sampuli ya kufundishia.

Dk amesema kuwa alikuwa akisumbuliwa na maumivu kwenye sehemu zake za siri hivyo ikambidi aende katika hospitali hiyo ili kupatiwa matibabu.

“Wakati nimelala katika  chumba cha kufanyiwa vipimo huku nikiwa mtupu waliingia Wasichana wawili ambao waliniambia kuwa wao kiumri ni wadogo sana kwangu kitu kilichonifanya nishituke sana” amesema DK

Aidha Dk anasema kuwa wakati akichukuliwa vipimo, Daktari aliwauliza maswali Wanafunzi hao wawili kitu kilichomfanya agundue kuwa amegeuzwa sampuli ya kufundishia bila yeye kujua.

Kwa sasa Dk ameifungulia mashtaka hospitali hiyo akidai afidiwe baada ya kugeuzwa sampuli ya kufundishia bila ridhaa yake huku hospitali hiyo ikitakiwa na mahakama kuleta utetezi wake Julai 18.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad