Kikao cha Mazishi ya Maria na Consolata Kinafanyika

Kikao cha Mazishi ya Maria na Consolata Kinafanyika
Kikao baina ya Serikali, Kanisa la Roman Katoliki na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha (Ruco) bado kinaendelea ili kupata muafaka wapi mazishi ya mapacha walioungana Maria na Consolata yatafanyika.

Hadi leo Juni 4, saa nne asubuhi bado hakuna ratiba wala mahali ambako msiba huo umewekwa.

Akizungumza na Mwananchi kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Richard Kasesela amesema taratibu zote zitawekwa hadharani baada ya kumalizika kikao hicho kinachofanyika Kanisa Katoliki, Jimbo la Iringa.

"Bado kikao kinaendelea, taratibu zote zitawekwa wazi tukishakubaliana," amesema.

Mapacha hao walifariki Juni 2, 2018 wakati wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa baada ya kurejeshwa toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Utility

1996-Mwaka waliozaliwa

2018-Wamefariki

Udzungwa Sekondari- Elimu ya Kidato cha tano na sita
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad