Kikwete, Mecky Sadick Wateuliwa Kamati Maalumu ya Kuivusha Yanga Kwenye Majanga Inayopitia

Klabu ya soka ya Yanga kupitia Mkutano wake Mkuu wa mwaka, uliofanyika kwenye Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam, imepitisha mabadiliko na kuteua kamati maalum kwaajili ya kuivusha timu.

Katika mkutano huo, Yanga wametangaza Bodi mpya ya wadhaamini inayoundwa na waliokuwepo awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala bora) George Mkuchika mke wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mama Fatma Karume, Francis Kifukwe, Jaji Mstaafu John Mkwawa pamoja na Mzee Katundu.

Mkutano huo pia umeridhia kuteuliwa kwa kamati maalum ya kuivusha timu hiyo kwenye kipindi hiki cha mpito inachopitia wakati mchakato wa kuweka namna nzuri ya uendeshaji ukiendelea. Kamati hiyo yenye watu 12 itaongozwa na Mwenyekiti Tarimba Abbas na Makamu Mwenyekiti Said Mecky Sadick.

Wajumbe 10 wa kamati hiyo ni Abdallah Binkleb, Nyika Hussein, Samwel Lukumay, Mashauri Lucas, Yusuphed Mhandeni, Hamad  Islam, Makaga Yanga, Ridhiwan Kikwete, Majid Suleiman na Hussein Ndama.

Yanga imekuwa kwenye wakati mgumu kiuchumi siku za hivi karibuni kiasi cha kufikia hatua ya kutofanya vizuri pamoja na kujitoa kwenye michuano ya CECAFA KAGAME CUP 2018
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad