Kim Nana Awatolea Uvivu Gigy Money na Lynn

Kim Nana Awatolea Uvivu Gigy Money na Lynn
VIDEO Queen Lilian Paul Kessy ‘Kim Nana’ amewafunda wauza nyago wenzake, Gift Stanford ‘Gigy Money’ na Irene Hillary ‘Lynn’ kuwa na staha mbele za watu kutokana na maneno machafu waliyokuwa wakitoleana mitandaoni kutokana na ugomvi wao uliotokea hivi karibuni.



kwamba watu wanawaangalia, maneno waliyokuwa wakirushiana yanafanya watu waidharau fani yetu na kuona kuwa ni ya kihuni kutokana na kuropoka ovyo mbele za watu,”

Akipiga stori na Udaku wa Mjini, Kim Nana alisema hakufurahishwa na wauza nyago hao kusemeana mbovu hadharani kwani ingekuwa vema wakaitana pembeni na kugombana pasipo kuwapa watu faida hasa ikichukuliwa kuwa, wao ni kioo cha jamii.



“Unajua wameshindwa kutambua kuwa wao ni kioo cha jamii na alisema Kim Nana.Gigy na Lynn juzikati walirushiana maneno ya shombo mtandaoni kisa kikiwa hakijulikani na hata mwandishi wetu alipojaribu kuwatafuta, hakuna aliyetoa ushirikiano
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad