Kimenuka! Mwimbaji wa Injili Kutoka Kenya Ataka Daimond Amwachie Zari " Nataka Kumuoa Tumtumikie Mungu"

Miezi minne baada ya ulimwengu kubaini kuhusu kuwachana kwa nyota wa muziki wa bongo Diamond Platinumz na mpenziwe Zari Hassan, msanii wa muziki wa Injili nchini Kenya Alex Apoko ,maarufu Ringtone ameonyesha hamu ya kumchumbia mama huyo wa watoto watano.

Rington anayejulikana kwa wimbo wake 'Tenda Wema' aliyeimba na msanii wa Tanzania Christine Shusho anasema kuwa yeye ndio suluhu kwa matatizo ya kimapenzi ambayo yamekuwa yakimzonga mfanyibiashara huyo wa Uganda.

Msanii huyo sasa amemtaka mfanyibiashara huyo kutokubali kumrudia Diamond Platinumz na badala yake kukubali uchumba wake kwa lengo la kumtumikia Mungu.

''Diamond aniwachie Zari, Zari ni wangu wa Moyoni, atuwache tumtumikie Mungu'', alisema Rington alipotembelea afisi mpya za BBC jijini Nairobi.

Msanii huyo anasema kwamba aliota ndoto siku ambayo wawili hao waliachana ambapo anadai kumuona Zari.

''Nilipoamka nikahisi moyo wangu unamtaka mwanamke huyu na sio mtu mwengine yeyote, hapo nilijiuliza maswali na nikasikia sauti upande mwengine ikiniambia usijali kile watu watakachozungumza fuata Moyo wako na usimkosee Mungu''.


Top Post Ad

Below Post Ad